Tuesday, October 15, 2013

MWANDISHI WA ITV UFOO SARO AJERUHIWA KWA RISASI, NA MAMA YAKE MZAZI AUAWA

 Mwandishi wa ITV na Radio one Ufoo Saro, ameripotiwa kupigwa risasi na mtu anayetajwa kuwa mzazi mwenzake, anayejulikana kwa jina la Mushi. Mushi ambaye alirejea Dar akitokea Dar fur, alidaiwa alishindwa kuelewana na mzazi mwenzake Ufoo, na kupelekea wawili hao kwenda kwa mama wa Ufoo anayeishi Kibamba, ili kuwapatanisha. Habari zinasema baada ya kushindwa kuelewana ndipo Mushi alipompiga mama wa Ufoo risasi kichwani na kufa papo hapo, na kumpiga Ufoo risasi mguuni na tumboni. Baada ya Mushi kudhani kuwa ameshawaua wote alijipiga risasi kidevuni, na yeye kufa papo hapo. Aidha Ufoo alipelekwa hospitali ya Tumbi, kwa msaada wa mwendesha pikipiki, na baadaye kuhamishiwa kwenye hospitali ya Muhimbili, anapoendelea na matibabu.

 Hapa mwandishi wa habari wa ITV, na REDIO ONE Ufoo Saro akirejeshwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Muhimbili.

 Hapa ni nyumbani kwa mama yake mzazi, ambaye alifariki baada ya kupigwa risasi. Hapa ndipo shughuli za mazishi zinafanyika.

No comments:

Post a Comment