Thursday, October 31, 2013

MWANAMKE AKAIDI AMRI YA POLISI, APIGWA RISASI MKOANI ARUSHA

                       Kamanda wa polisi mkoa wa ARUSHA Liberatus Sabasi.

Mwanamke mkazi wa PPF jijini Arusha Vaileth Mathias amepigwa risasi na polisi na kujeruhiwa eneo la benki ya CRDB Mapato, baada ya kukaidi amri halali ya polisi na kumtishia silaha. Tukio hilo lilitokea jana saa 7 mchana katika benki hiyo ya CRDB tawi la mapato, mkabala na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Arusha.

Vaileth alifika eneo hilo akiwa na gari aina ya toyota cresta namba T 888 BWW, na kutaka kuliegesha katika lango la kuingilia magari ya kuchukua, na kupeleka fedha katika benki hiyo. Asikari polisialiyekuwa akilinda eneo hilo alimwamuru Vaileth kutoegesha gari eneo hilo lakini akapuuza, na kukaidi kisha akaingia ndani ya benki na askari huyo akaamua kutoa upepo kwenye matairi ya gari hilo.
Vaileth alipotoka ndani ya benki alienda kwenye gari lake na kukuta matairi hayana upepo, naye kwa hasira akamkabili askari polisi aliyekuwa lindoni huku akimtolea maneno ya " Hata kama una bastola
nami ninayo" na kuitoa na kukoki akitaka amshambulie askari.

Hata hivyo askari alimwahi kwa bastola na kumpiga begani na kumfanya aanguke chini na bastola yake kumtoka mkononi. alisema kamanda wa polisi Arusha, huku akiwataka wananchi kutii sheria bila shuruti,na kusema mwanamke huyo alivunja sheria kwa kukaidi amri ya polisi, na hakuna aliyejua lengo lake lilikuwa ninini.
Mwanamke huyo alipelekwa hospitali ya Mount meru, na baadaye kupelekwa selian kwaajili ya kufanyiwa matibabu ya kutolewa risasi.

No comments:

Post a Comment