Thursday, October 31, 2013

MWANAMKE AKAIDI AMRI YA POLISI, APIGWA RISASI MKOANI ARUSHA

                       Kamanda wa polisi mkoa wa ARUSHA Liberatus Sabasi.

Mwanamke mkazi wa PPF jijini Arusha Vaileth Mathias amepigwa risasi na polisi na kujeruhiwa eneo la benki ya CRDB Mapato, baada ya kukaidi amri halali ya polisi na kumtishia silaha. Tukio hilo lilitokea jana saa 7 mchana katika benki hiyo ya CRDB tawi la mapato, mkabala na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Arusha.

Vaileth alifika eneo hilo akiwa na gari aina ya toyota cresta namba T 888 BWW, na kutaka kuliegesha katika lango la kuingilia magari ya kuchukua, na kupeleka fedha katika benki hiyo. Asikari polisialiyekuwa akilinda eneo hilo alimwamuru Vaileth kutoegesha gari eneo hilo lakini akapuuza, na kukaidi kisha akaingia ndani ya benki na askari huyo akaamua kutoa upepo kwenye matairi ya gari hilo.
Vaileth alipotoka ndani ya benki alienda kwenye gari lake na kukuta matairi hayana upepo, naye kwa hasira akamkabili askari polisi aliyekuwa lindoni huku akimtolea maneno ya " Hata kama una bastola
nami ninayo" na kuitoa na kukoki akitaka amshambulie askari.

Hata hivyo askari alimwahi kwa bastola na kumpiga begani na kumfanya aanguke chini na bastola yake kumtoka mkononi. alisema kamanda wa polisi Arusha, huku akiwataka wananchi kutii sheria bila shuruti,na kusema mwanamke huyo alivunja sheria kwa kukaidi amri ya polisi, na hakuna aliyejua lengo lake lilikuwa ninini.
Mwanamke huyo alipelekwa hospitali ya Mount meru, na baadaye kupelekwa selian kwaajili ya kufanyiwa matibabu ya kutolewa risasi.

Sunday, October 20, 2013

MTANGAZAJI MKONGWE HAPA NCHINI JULIUS NYAISANGA AFARIKI DUNIA LEO 20/10/2013

 Mtangazaji mkongwe hapa nchini Ndg. Julius Nyaisanga a.k.a. Ancle J, ameripotiwa kufariki dunia alfajiri ya  leo 20/10/2013, katika hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro. Akidhibitisha kifo hicho kaimu meneja wa kituo cha Abood Media Ndg. Abeid Dogoli, amesema Julius Nyaisanga ambaye alikuwa mfanyakazi katika kituo hicho kama meneja wa kituo, alipelekwa hospitalini hapo jana mchana akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na presha. Julius Nyaisanga ambaye alishawahi kuwa mtangazaji wa radio tanzania, na radio one, amefariki akiwa na umri wa miaka 53.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA NGULI WA UTANGAZAJI UNCLE J. AMEN.

Julius Nyaisanga katikati, akiwa na mtangazaji Liongo wakwanza kushoto, enzi za uhai wake.

Tuesday, October 15, 2013

MWANDISHI WA ITV UFOO SARO AJERUHIWA KWA RISASI, NA MAMA YAKE MZAZI AUAWA

 Mwandishi wa ITV na Radio one Ufoo Saro, ameripotiwa kupigwa risasi na mtu anayetajwa kuwa mzazi mwenzake, anayejulikana kwa jina la Mushi. Mushi ambaye alirejea Dar akitokea Dar fur, alidaiwa alishindwa kuelewana na mzazi mwenzake Ufoo, na kupelekea wawili hao kwenda kwa mama wa Ufoo anayeishi Kibamba, ili kuwapatanisha. Habari zinasema baada ya kushindwa kuelewana ndipo Mushi alipompiga mama wa Ufoo risasi kichwani na kufa papo hapo, na kumpiga Ufoo risasi mguuni na tumboni. Baada ya Mushi kudhani kuwa ameshawaua wote alijipiga risasi kidevuni, na yeye kufa papo hapo. Aidha Ufoo alipelekwa hospitali ya Tumbi, kwa msaada wa mwendesha pikipiki, na baadaye kuhamishiwa kwenye hospitali ya Muhimbili, anapoendelea na matibabu.

 Hapa mwandishi wa habari wa ITV, na REDIO ONE Ufoo Saro akirejeshwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Muhimbili.

 Hapa ni nyumbani kwa mama yake mzazi, ambaye alifariki baada ya kupigwa risasi. Hapa ndipo shughuli za mazishi zinafanyika.

Sunday, October 13, 2013

BANANA INVESTMENTS YASHIRIKI MAANDAMANO YA KUPINGA UJANGILI WA TEMBO NCHINI TANZANIA

Yalikuwa ni maandamano makubwa yaliyoandaliwa kupinga uwindaji haramu, na ujangili wa kuua tembo katika nchi ya Tanzania. Maandamano yalianzia kwenye ofisi za Tanapa mjini Arusha na kuhitimishwa kwenye viwanja vya AICC club Kijenge. Waziri wa maliasili na utalii Mh. Hamisi Kagasheki alihutubia wananchi katika viwanja hivyo. Aidha maandamano kama haya yalifanyika katika nchi zingine, ikiwemo China na Marekani kuonyesha kuwa wanapinga ujangili wa tembo duniani. Kampuni ya Banana Investments kwa kutambua umuhimu wa kuhifadhi mali asili za taifa letu, ilishiriki katika maandamano hayo kwa kutuma wawakilishi wake katika maandamano, kama wanavyoonekana kwenye picha hapo chini wakiwa wamevalia t-sheti za kinywa chake cha Fiesta dry gin kinachoongoza katika soko la Tanzania.


Friday, October 11, 2013

ANGALIA SIKU WAFANYAKAZI WA BANANA INVESTMENTS LTD, WALIPOSHIRIKI MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON

 Wafanyakazi wa banana investments wakiwa pamoja muda mfupi kabla ya kuanza mashindano ya Kil marathon km 21, na km 5
 Baadhi ya wafanyakazi wa banana investments wakiwa katika mbio za km 21. (Half marathon)
 Hapa mkurugenzi mtendaji wa banana investments Ndg. A. R. Olomi, wa tatu kutoka kulia akiwa katika mbio za km 21.
 Hapa washiriki wakisubiri kupatiwa medali zao baada ya kumaliza mbio za km 21.
 Ndugu Steven Mvungi wa kwanza toka kulia, na ndugu John Mgonja wote wakiwa wafanyakazi wa banana investments, wakiwa na medali baada ya kumaliza mbio za km 21
 Wafanyakazi wa banana investments baada ya kurejea kiwandani, wakiwa na furaha, baada ya kumaliza mashindano.
Picha ya pamoja baada ya kurejea kiwandani.

Tuesday, October 1, 2013

KAMPUNI YA BANANA YAFANYA MKUTANO NA SHEREHE KABAMBE KWA MAWAKALA WAKE MKOA WA TANGA 2013

 Mkurugenzi mtendaji wa Banana Investments Ndg. Adolf R. Olomi, akitoa semina ya ujasiriamali kwa mawakala wa kampuni mkoa wa Tanga, kwenye sherehe walioandaliwa na kampuni.
 Meneja masoko wa Banana Investments Ndg. David Damian, akitoa somo kwa mawakala mkoa wa Tanga kuhusu utaratibu wa kutoa motisha (Bonus) kwa mawakala wanaofanya vizuri katika mauzo.
 Ngugu Respics Ndukya wakala wa Banana Investments kutoka Korogwe, akiwa ameshikilia Tv bapa yeye na mke wake, ikiwa ni zawadi kwao ya mshindi wa kwanza katika mauzo ya mwaka 2013 kwa mawakala wa mkoa wa Tanga.
 Hapa meneja mauzo wa Banana Investments Ndg. Elisante Makyao, akionyesha baiskeli ambayo ni zawadi ya mshindi wa tatu kwa mawakala mkoa wa Tanga ambaye hakufanikiwa kuhudhuria katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi mtendaji wa Banana Investments, aliyevaa miwani, na meneja mauzo bohari ya Tanga wakimkabidhi Ndg. Materu wa Tanga mjini aliyeshika bahasha zawadi ya TV kichogo, ikiwa ni zawadi ya mshindi wa pili kimauzo kwa mawakala wa mkoa wa Tanga.
 Mmoja wa mawakala mkoa wa Tanga, akipokea zawadi ya saa toka kwa mkurugenzi mtendaji wa Banana Investments, zawadi za saa zilitolewa kwa mshindi wa nne hadi wa kumi na tatu kimauzo.
 Burudani ya muziki pia ilikuwepo, hapa wacheza show wa kundi la promotion la Banana Investments, wakitoa burudani katika sherehe hiyo ya mawakala wa kampuni mkoa wa Tanga.
 Hapa burudani kabambe ikiendelea kutoka kwa mcheza show mahiri Ndg. Tompoo kuwaburudisha wageni.
 Vyakula vya kila aina viliandaliwa, hapa mkurugenzi mtendaji wa Banana Investments akichota chakula kuashiria kuwakaribisha wageni kupata chakula wakati wa sherehe.
 Vinywaji vya kila aina vilikuwepo ndani ya ukumbi, vikiongozwa na vinywaji bora vinavyozalishwa na kampuni ya Banana Investments, ambavyo ni Raha, Raha poa na Fiesta dry gin.

Hapa mawakala wakifurahia jambo wakati wa sherehe yao waliyoandaliwa na kampuni, huku wakifurahia vinywaji bora vinavyozalishwa na kampuni ya Banana Investments.

Banana Investments iliposhiriki maonesho ya kimataifa ya biashara mkoani Tanga 2013

 Waziri wa viwanda na biashara. Mh. Abdalah Kigoda akihutubia washiriki wakati akifungua rasmi maonesho ya kimataifa ya biashara mkoani Tanga
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa, akihutubia washiriki wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kimataifa ya biashara Tanga
 Waziri wa viwanda na biashara alipotembelea banda la bidhaa za Banana investmetns wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara mkoani Tanga. Hapa akipata maelezo toka kwa meneja mauzo mkoa wa Tanga.
 Mbunge wa Lushoto mjini Mh. Hendri Shekifu akipata maelezo juu ya bidhaa za Banana Investments, toka kwa mwakilishi wa kampuni S. Mvungi wakati wa maonesho.
 Mkurugenzi mtendaji wa Banana investments, wa pili kutoka kushoto Mh. Adolf R. Olomi akiwa na viongozi wengine wa kampuni walipotembelea banda la kampuni wakati wa maonesho.
 Hiki ndicho cheti cha ushindi wa pili ambacho kampuni ya Banana Investments ilishinda wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara mkoani Tanga
 Muonekano wa banda la Banana investments ndani ya banda kuu la maonesho (Excecutive Tent)
 Bidhaa zikiwa zinapendeza ndani ya banda wakati wa maonesho.
 Wateja wa bidhaa za Raha, Raha poa, na Fiesta dry gin zinazozalishwa na kampuni ya Banana Investments wakionja bidhaa hizo wakati wa maonesho.
 Ilikuwa ni burudani mwanzo mwisho, hakika kila mmoja aliyetembelea banda la Banana Investments alifurahi.
 Hapa wateja wakipata maelezo juu ya bidhaa za kampuni toka kwa meneja mauzo wa bohari ya Tanga. Ndg. Adolf Nikolao Mlay
 Kushoto ni meneja wa  PPF kanda ya Kinondoni, Pwani na Tanga, Bi. Zahra R. Kayugwa, alipotembelea banda la Banana Investments wakati wa maonesho.
 Banda la Banana Investments likiwa linapendeza wakati wa maonesho.
 Madhari tulivu ya bahari ya hindi Mkoani Tanga, meli kwa mbali ikikaribia kuingia bandarini.
Waziri wa viwanda na biashara Mh. Abdalah Kigoda alipokata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa maonesho ya kimataifa ya biashara mkoani Tanga.