Hapa wakipozi baada ya kifungua kinywa, na kujinunulia mahitaji muhimu njiani wakati wa safari
Safari ikaanza baada ya kifungua kinywa kuelekea hifadhi ya SAADAN.
Baada ya safari ya kutwa nzima sasa ndani ya saadan, na tayari hapa tent zimeshaandaliwa kwa ajili ya malazi
Siku iliyofuata safari ya kutembelea vivutio ndani ya hifadhi ilianza. hapa picha ya pamoja kwenye mbuyu uliotumiwa na wajerumani kuwanyongea mababu zetu enzi za ukoloni.
Hapa baadhi ya wanachama wakijipumzisha baada ya kutoka kutembelea vivutio ndani ya hifadhi
Baada ya safari kuzunguka hifadhi sasa ni picha ya pozi karibu na bahari ya hindi
Misosi ilikuwa ya kutosha kabisa, hapa warembo wakijipatia maakuli, ndani ya hifadhi ya saadani
Mlango huu uliachwa na waarabu waliotumia majengo haya ndani ya hifadhi ya saadani. Mlango huu upo hivihivi tangu mwaka 1700, hadi leo.
Haya ni mabaki ya stoo iliyotumiwa na waarabu ndani ya hifadhi ya saadani, tangu mwaka 1700.
Hakika maji ya mto yanatisha. Eneo hili ndipo maji ya mto WAMI yanapokutana na maji ya bahari ya HINDI. wanachama wa banana sport club walitumia boti hii kufika katika eneo hili.
Ndani ya bahari ya hindi, ilikuwa tukio la kihistoria na la kishujaa kuwa ndani ya maji haya kwa kutumia boti. Hapa boti inapishana na viboko, na mamba.
Ha.pa nahodha wa boti akiongoza boti, pamoja kutoa maelezo kwa wanachama wa banana sport club
Wengi waliogopa safari hii ndani ya maji, ila walijipa moyo na baada ya kurejea nchi kavu walipongezana kwa kufanikisha tukio hili la kihistoria katika maisha yao.
Hapa ni kwenye kivuko cha pangani, pia ni eneo maji ya mto pangani yanakutana na maji ya bahari ya hindi.
Hili ni yai la kasa likiwa limefukiwa kwaajili ya kutotolewa pembeni ya bahari ya hindi ndani ya hifadhi ya saadan. Kasa hutaga mayai nje ya maji na kuyafukia hadi yanapoanguliwa na vitoto hurejea baharini.
Amini usiamini mnyama Nguruwe huishi katika makazi ya watu ndani ya hifadhi ya saadan, katika kijiji cha saadani.
Katika kivuko cha pangani wakati wakurudi Arusha kutokea hifadhi ya Saadani.
NB: Shukrani ziwaendee waandaaji wa safari hii kwa kuwa na wazo hili na kulifanyia kazi hatimaye kuandaa safari hii. Waliofanikisha safari hii ni MOSES JANUARY na ALBINA ANTHON, hongereni sana. Pia shukrani za pekee ziwaendee viongozi, na wakurugenzi wa Banana investments kwa kuwaruhusu wafanyakazi hao, ambao ni wanachama wa banana sport club, kufanya safari hii. MUNGU AWABARIKI WOTE
